MSTAHIKI
Meya wa jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita leo amewasilisha mpango wa
bajeti wa mwaka 2018 hadi 2019 ambapo jumla ya shilingi bilioni 75.2
zitatumika kwa mwaka huo.
Hata hivyo mpango huo umepitishwa kwa kauli moja na Madiwani wote wa halmashauri hiyo huku wakimpongeza kwa kusema kuwa jiji limepata Meya anayejali maslahi ya maendeleo katika halmashauri hiyo.
Halmashauri
hiyo imeandaa mpango huo kwa kuzingatia taratibu zinazotakiwa kufuatwa
na mamlaka za Serikali za mitaa katika utayarishaji wa makadirio ya
mapato na matumizi ya mwaka wa fedha wa 2018 na 2019.
Akizungumzia mpango
huo kwenye mabaraza la Madiwani na waandishi wahabari , Meya Mwita
amesema kuwa jiji limekadiria kukusanya na kutumia shilingi bilioni 75.2
ambapo itatokana kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo bilioni 18.1 zinatarajiwa kukusanywa kutoka kwenye vyanzo vya vyandani.
Aidha amefafanua kuwa mapato mengine yatapatikana kutokana na halmashauri kubuni vyanzo vingine vya mapato sambamba na kuboresha mikakati ya ukusanyaji wa mapato.
Amefafanua
kuwa utekelezaji wa bajeti hiyo umelenga kutekelaza mradi wa ujenzi wa
kituo cha mabasi cha Mbezi Luis,kuboresha miundombinu ya Dampo,ujenzi wa
vyoo vya Umma na kuhakikisha utoaji wa huduma usiokua na usumbufu kwa
wananchi.
Amesema halmashauri pia imepanga kutumia asilimia 65 ya mapato ya
ndani sawa na shilingi bilioni 11.7 kwa ajili ya kuchangia miradi
mbalimbali ya maendeleo ,shilingi bilioni 1.08 zitatumika kwa ajili ya
mfuko wa wanawake ,vijana na walemavu.
Akizungumzia suala la utalii ,Meya Mwita amesema kuwa katika bajeti hiyo zaidi
ya bilioni mbili zimetengwa ili kuboresha sekta ya hiyo ikiwemo kununua
mabasi ,kutengeneza na kuboresha vivutio mbalimbali vilipo jijini hapa.
Ameongeza kua kuboreshwa kwa sekta hiyo kutaongezea pato la Taifa pamoja na kutoa ajira kwa vijana waliosomea masuala ya utalii ambao kwa kiasi kikuba hawana ajira.
“
Kama jiji la Dar es Salaam tumeona ni wakati muafaka sasa wakuweka
nguvu kwenye sekta ya utalii, ambayo kwa kiasi kikubwa kitakuwa ni
kivutio kwa wageni kuja hapa ,maanye ni kwamba jiji litapata fedha
nyingi kupitia mpango huo” amesema Meya Mwita.
Imetolewa leo Februali 24
Na Christina Mwagala Afisa habari Ofisi ya Meya wa jiji.
0 comments:
Post a Comment