Dar es salaam Yetu
  • Home
skip to main | skip to sidebar

MALKIA NA BALKIA WACHANGAMKIA FURSA YA KUJIWEKEA AKIBA NA NSSF

Katika kuelekea kilele cha Malkia wa Nguvu 2025 inayoratibiwa na Chombo cha Clouds.

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umewafikia Malkia na Balkia katika Soko la Kariakoo, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa elimu, kuandikisha wanachama wapya waliojiajiri ili waweze kujiunga na kujiwekea akiba kwa kuchangia shilingi 30,000 au zaidi kwa kutoa kidogo kidogo kwa siku bukubuku, wiki, mwezi au msimu kulingana na kipato chake na hapo baadae wote watakuwa wanufaika ws mafao yote yanayotolewa na NSSF yakiwemo ya uzee, uzazi na matibabu.

Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Clouds Fm,  Bw. Shabani Mbwana, Afisa Matelekezo Mkuu wa NSSF, amesema lengo la kuanzishwa kwa Mfuko ni kuhakikisha wananchi wanapata kinga dhidi ya majanga kama uzee au kupungua kwa kipato ambapo mtu anayejiwekea akiba anapopatwa na majanga ya aina hiyo atanufaika na mafao kutoka NSSF. Aidha, amesema kuwa Mfuko umeanzisha Skimu maalumu kwa ajili ya wananchi waliojiajiri hivyo amewataka kujiunga na kuchangia ili wawe Mastaa wa Mchezo pale watakaposhindwa kufanya kazi za uzalishaji mali waweze kunufaika na mafao na huduma nyingine zinazotolewa NSSF.












at 10:15 PM 0 comments
Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook

Rais Samia akutana na kuzungumza na viongozi pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA)




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

 Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye 

mazungumzo na viongozi pamoja na wajumbe wa 

 Bodi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi 

Zanzibar (ZEEA) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Machi, 2025. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia
 Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na viongozi pamoja
 na wajumbe wa  Bodi ya Wakala wa Uwezeshaji 
Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) Ikulu Jijini
 Dar es Salaam tarehe 26 Machi, 2025.


at 7:50 PM 0 comments
Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook

Rais Samia apokea Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. Félix Tshisekedi Ikulu Jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan 
akiwa kwenye mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya
 Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi ambaye ni
 Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi hiyo Mhe. Thérèse Kayikwamba Wagner, 
Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Machi, 2025.
at 7:44 PM 0 comments
Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook

DAWASA YAPEWA SIKU 90 KUTATUA CHANGAMOTO YA MAZINGIRA FUKWE YA DENGU


Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA)

 imepewa siku 90 kuhakikisha adha ya uchafuzi wa

 mazingira inayosababishwa na uunganishaji wa

 mifumo ya maji kiholela fukwe ya Dengu na Fukwe ya Barabara ya

 Obama jirani na 

Hospitali ya Aghakan jijini Dar es Salaam inatatuliwa.

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 26 Machi, 2024 na Naibu Katibu Mkuu ofisi ya 

Makamu wa Rais (Mazingira) Bi. Christina Mndeme alipokuwa akiongea na 

Waandishi wa Habari katika ziara yake iliyohudhuriwa pia na Baraza la Taifa 

la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) la kuhakikisha DAWASA

 wanajenga eneo la kutibu maji kabla ya kuingia baharini ili kulinda Afya ya 

viumbe wa baharini na Ikolojia ya bahari kwa ujumla.


at 7:42 PM 0 comments
Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook

RAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA DC MASASI! MOBHARE MATINYI APEWA UBALOZI SWEDEN


at 6:46 AM 0 comments
Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook

MKURUGENZI MKUU NSSF AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA UGANDA

MKURUGENZI MKUU NSSF AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA UGANDA

Na Mwandishi Wetu,

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Masha Mshomba, tarehe 27 Januari 2025 amekutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Robinah Nabbanja Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kikao, Bw. Mshomba amesema Mhe. Robinah Nabbanja amefika nchini kwa lengo kuhudhuria Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika ambapo mbali na mkutano huo aliona ni vizuri kukutana na NSSF kwa lengo la kufahamu mambo kadhaa kuhusu utendaji wa Mfuko ikiwa pamoja na suala la ukuaji wa thamani ya Mfuko, uwekezaji, usajili wa wanachama wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi na ulipaji wa mafao ya wanachama ili kupata uzoefu.

“Kama tunavyofahamu nchi yetu ya Tanzania imepata heshima kubwa kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Uganda amefika hapa nchini kwa lengo la kuhudhuria mkutano huo, lakini ameona ni vizuri kuja kukutana na NSSF kwa lengo la kufahamu masuala kadhaa ya utendaji ikiwemo uwekezaji unaofanywa na NSSF, ulipaji wa mafao na masuala mengine ya huduma ikiwemo ushirikiano kati ya NSSF Tanzania na ile ya Uganda' na kwa kweli tumezungumzia hayo ambayo aliomba tuyazungumzie na tumemueleza kwa mfano uwekezaji wetu katika dhamana za Serikali, uwekezaji kwenye miundombinu mfano wa Daraja la Nyerere Kigamboni, Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi kule Morogoro na miradi mengine ambayo NSSF imewekeza ikiwa ni pamoja na ile ya majengo” alisema Bw. Mshomba.

Bw. Mshomba pia alimueleza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Uganda kuwa NSSF ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, hususani kitengo cha Hifadhi ya Jamii pamoja na Benki Kuu ya Tanzania na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwenye masuala ya uwekezaji.

Vile vile, Bw. Mshomba alisema Mfuko umeimarika sana katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipoingia madarakani.

“Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, NSSF imepata mafanikio makubwa ya utendaji hii inatokana na juhudi kubwa sana ya serikali yake katika kuvutia wawekezaji nchini," alisema Bw. Mshomba.

Alisema kwa sababu NSSF inawafikia waajiri na wajiriwa katika sekta binafsi na pia sekta isiyo rasmi, hivyo wawekezaji wanavyokuja nchini, inapelekea ongezeko la wanachama, inaongeza waajiri, na hivyo kuongeza michango. Aidha, uwekezaji na mapato yanayotokana na uwekezaji yamekuwa yakiongezeka.

Bw. Mshomba alimueleza Mhe. Robinah Nabbanja kuwa NSSF imeruhusiwa kuwekeza nje ya nchi katika eneo la Afrika Mashariki, pia katika eneo la SADC, ambapo kwa uwekezaji huo utasaidia kuongeza mapato ya NSSF kupitia uwekezaji huo.

“Katika uwekezaji huo tulioruhusiwa kuwekeza nje ya nchi, NSSF tumekuwa tukishirikina na Mifuko mingine ya Hifadhi ya Jamii, mfano wenzetu wa NSSF Uganda tunapofikiria kuwekeza katika HISA nchini Uganda ni lazima tushirikiane nao kupata uzoefu wao katika soko la HISA la Uganda," alisema Bw. Mshomba.

Kwa upande wa ushirikiano katika ya Mifuko miwili ya NSSF Tanzania na NSSF Uganda ni mzuri kwani NSSF Tanzania imekuwa ikiwapa ushirikiano mzuri NSSF Uganda hasa wanapokuja kuwekeza Tanzania, ambapo wao wameanza kuwekeza katika dhamana za Serikali kwa muda mrefu.

“ Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Uganda amefurahi sana kuona ushirikiano uliopo na wenzetu wa NSSF  Uganda na akatoa rai kuwa ni vizuri tukaendeleza ushirikiano huo kwa sababu si tu unajenga hizi taasisi mbili bali unajenga nchi na unaimarisha uhusiano katika nchi na nchi kitu ambacho ni muhimu hasa tunapofikiria kuendeleza Jumuiya ya Afrika Mashariki na hilo amesisitiza sana na akaahidi atakaporudi nchini Uganda ataweka msisitizo katika hilo.” aliongeza Bw. Mshomba

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Robinah Nabbanja aliipongeza NSSF kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuwahudumia wanachama na Taifa kwa ujumla na kuomba ushirikiano uendelee kwa maslahi mapana ya nchi zote mbili.





at 4:28 PM 0 comments
Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook

MENEJA NSSF KINONDONI AWATAKA WAJASIRIAMALI KUENDELEA KUJIUNGA NA KUJIWEKEA AKIBA ILI WAWEZE KUNUFAIKA NA MAFAO


Meneja wa NSSF Mkoa wa Kinondoni, Bw. Large Materu ametoa wito kwa wajasiriamali kuendelea kujiunga na kujiwekea akiba katika Mfuko ili waweze kunufaika na mafao yanayotolewa yakiwemo ya uzee, uzazi na matibabu.

Alitoa wito huo wakati akiongoza utoaji wa elimu ya hifadhi ya jamii kwa viongozi wa masoko na baadaye  wafanyakazi wa NSSF waliweka kambi kwenye masoko ya Kawe na Tegeta Nyuki kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii, kuandikisha wanachama wapya, kuhamasisha uchangiaji ambapo hamasa ya wajasiriamali kupata elimu na kujiunga imekuwa kubwa. 

“Napenda kutoa wito kwa wajasiriamali wote wakiwemo mama lishe, bodaboda, wakulima, wafugaji, wavuvi kuwa NSSF ndio Mfuko wao, hivyo waendelee kujiunga na kujiwekea akiba ili waweze kunufaika na mafao yote kama vile ya uzee, urithi, uzazi na matibabu,” alisema.

Bw. Materu alisema NSSF imeweka utaratibu mzuri wa wajasiriamali kujiunga na kuchangia ambapo mwanachama baada ya kujiandikisha anapewa namba ya kumbukumbu ya malipo na anapaswa kuchangia kuanzia shilingi 30,000 au 52,200 au zaidi kwa mwezi na anaweza kuchangia kidogo kidogo kwa siku, wiki au mwezi ili aweze kunufaika na mafao hayo.

Aidha, alisema NSSF imepiga hatua kubwa katika utoaji wa huduma kwa wanachama na wananchi kwa kutumia mifumo ya TEHAMA ambayo inarahisisha huduma. "Tunaishukuru Menejimenti ya NSSF kwa kuweka nguvu kubwa sana katika kubadilisha mwelekeo wa utendaji kazi kuwa wa kidijitali zaidi ambapo imepelekea wanachama na wananchi kwa ujumla kupata huduma hukohuko waliko bila ya kulazimika kufika katika ofisi za NSSF," alisema Bw. Materu.

Alisema hayo ni mafanikio makubwa na kuwa lengo la NSSF ni kuendelea kufanya maboresho zaidi ya mifumo ili kumuwezesha mwanachama aweze kufungua madai ya mafao yake kwa njia ya mtandao bila ya kulazimika kufika kwenye ofisi za Mfuko.


 


at 1:13 PM 0 comments
Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook

WAJASIRIAMALI SOKO LA TEGETA NYUKI WANUFAIKA NA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII KUTOKA NSSF


Na MWANDISHI WETU,

Dar es Saalam. Lengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kufikisha elimu ya hifadhi ya jamii kwa makundi mbalimbali ya wananchi linaendelea kwa kasi baada ya wajasiriamali katika soko ya Tegeta Nyuki, jijini Dar es Salaam, kuhamasika kujiwekea akiba baada ya kupata elimu kutoka NSSF ili waweze kunufaika na mafao.

NSSF kupitia kwa Meneja wa Sekta isiyo rasmi, Bi. Rehema Chuma imeweka kambi ya siku nne katika soko la Tegeta Nyuki na Kawe, lengo likiwa ni kutoa elimu ya hifadhi ya jamii, kuandikisha wanachama wapya na kuhamasisha uchangiaji ambapo hamasa ya wajasiriamali kupata elimu na kujiunga imekuwa kubwa.

Akizungumza tarehe 8 Januari 2025, Bi. Rehema amesema katika muendelezo wa utoaji elimu kwa wajasiriamali NSSF imefika katika soko la Tegeta Nyuki kwa ajili ya kufikisha elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kujiunga na kujiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye.

Amesema kuna namna mbili za mwanachama kujiunga moja wapo ni kujaza fomu na mwenye namba ya NIDA anaelimishwa kujisajili kwa kutumia mifumo, na kuwa mwanachama anaweza kuwasilisha michango kupitia simu ya kiganjani huko huko aliko ambapo kima cha chini cha kuchangia ni shilingi 30,000 ambapo atanufaika na fao la matibabu.

Baadhi ya wajasiriamali akiwemo Pastory Anthony ambaye ni mwanachama wa NSSF ananufaika na mafao yanayotolewa na Mfuko ikiwemo ya matibabu pamoja na familia yake.

Amesema kuna faida nyingi ambazo anazipata kwa kuwa mwanachama wa NSSF hivyo amewaomba wajasiriamali wengine kujiwekea akiba NSSF kwani ni mkombozi kwa kila mwanachama.

Naye, Bw. Marc Donald Maganga, Afisa Mkuu wa Sekta isiyo rasmi, amesema NSSF imeweka utaratibu nzuri wa wajasiriamali kujiunga na kuchangia ambapo mwanachama baada ya kujiandikisha anapewa namba ya kumbukumbu ya malipo na anapaswa kuchangia kuanzia shilingi 30,000 au 52,200 au zaidi kwa mwezi na anaweza kuchangia kidogo kidogo kwa siku, wiki, mwezi, muhula au msimu ili aweze kunufaika na mafao yote yanayotolewa ikiwemo ya uzee, urithi, uzazi, matibabu na msaada wa mazishi.




at 9:04 AM 0 comments
Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook

TANZANIA NA UINGEREZA KUSHIRIKIANA KATIKA KUENDELEZA MADINI MKAKATI



▪️Waziri Mavunde ainisha Mkakati wa uongezaji thamani Madini

▪️Taasisi za Jiolojia na Utafiti Madini za Tanzania na Uingereza kushirikiana

▪️Watanzania kujengewa uwezo kukuza ujuzi

📍Dar es Salaam

Serikali ya Tanzania imeihakikishia Serikali ya Uingereza kuendeleza ushirikiano kwenye sekta ya madini hususani katika kujengea uwezo watu wake, kubadilishana uzoefu, uongezaji thamani madini na kuwekeza kwenye kufanya tafiti mbalimbali ili kukuza sekta ya madini na kupanua mnyororo wa thamani ili kuongeza ajira na kuchangia katika ukuaji wa pato la taifa.

Hayo, yameelezwa Jana na Waziri wa Madini, Mh. Anthony Mavunde katika ofisi ndogo za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Marianne Young.

"Kwanza kabisa Mhe. Balozi Young amefika ofisini kujitambulisha kwakuwa ana muda mfupi nchini tangu awasili lakini pia tumezungumzia ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Tanzania na Uingereza.

Katika mazungumzo hayo, Tanzania na Uingereza zimekubaliana katika kuwajengea uwezo watu wake na kubadilishana uzoefu hususani katika Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini nchini (GST) na British Geological Survey (*BGS*)ya Uingereza ili kuwajengwa uwezo Watanzania kwakuwa na ujuzi stahiki katika masuala ya uendelezaji wa sekta ya madini

Eneo la pili tulilozungumzia kwa urefu ni katika madini mkakati ambapo Uingereza wameonesha utayari katika kushirikiana na Tanzania katika eneo la mnyororo mzima wa uongezaji thamani madini mkakati ambapo Tanzania imejipanga kuhakikisha inavutiwa uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani madini hapa nchini.

Sasa ni muda muafaka wa kuhakikisha madini ya kimkakati yanawanufaisha Watanzania na taifa, na ndiyo maana tumeandaa Mkakati maalumu wa kutekeleza azma hiyo huku ikizingatiwa kuwa madini hayo kwa sasa yana mahitaji makubwa duniani.

Tupo katika hatua za mwisho kukamilisha mkakati huu maalum wa madini mkakati na muhimu ambao pia ni sehemu ya Kampeni ya Dunia katika kupunguza hewa ya ukaa kupitia matumizi ya nishati safi," amesema Waziri Mavunde.

Akizungumza katika Mkutano huo Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mh. Marriane Young amesema Uingereza inapongeza jitihada kubwa za kukuza sekta ya madini zinazofanywa na serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan na kuahidi kuimarisha ushirikiano mkubwa baina ya nchi hizi hasa katika kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo kupitia Taasisi za madini nchini Uingereza na Tanzania.

Balozi Young ameunga mkono mpango wa uongezaji thamani madini nchini na kuahidi kwamba Uingereza itashirikiana na Tanzania kwa ukaribu ili malengo hayo yatimie.
at 5:02 PM 0 comments
Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook

UCHUMI WA TANZANIA UNATARAJIWA KUKUA KWA ASILIMIA 5.7 KATIKA ROBO YA NNE YA MWAKA 2024


NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

UCHUMI wa Tanzania Bara na Zanzibar umeendelea kuwa imara kwa mwaka 2024 ambapo Uchumi wa Tanzania Bara ulikua kwa asilimia 5.4 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2024, na unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.6 katika robo ya tatu na asilimia 5.7 katika robo ya nne ya mwaka 2024.  

Kwa kuzingatia mwenendo huo, ukuaji wa uchumi unatarajiwa kuwa sawia na matokeo ya ukuaji wa asilimia 5.4 kwa mwaka 2024.

Hayo yameelezwa leo Januari 8, 2025 na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha robo mwaka cha Kamati ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania kufanyika na kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini.

Amesema ukuaji huu umechangiwa zaidi na ongezeko la shughuli za kilimo, usafirishaji, ujenzi, na biashara ambapo kwa upande wa Zanzibar, uchumi ulikua kwa asilimia 6.8 katika robo ya kwanza na asilimia 7.2 katika robo ya pili ya mwaka 2024, na unakadiriwa kukua kwa viwango hivyo kwa robo mbili zinazofuata, hivyo kufikia maoteo ya ukuaji wa asilimia 7.2 kwa mwaka 2024. 

Aidha Tutuba amesema katika mwaka 2025, ukuaji wa uchumi kwa Tanzania Bara na Zanzibar unatarajiwa kuendelea kuwa wa kasi ya kuridhisha, kwa takriban asilimia 6 na asilimia 6.8, mtawalia. 

"Ukuaji huu unatarajiwa kuchangiwa na ongezeko la uzalishaji katika shughuli za kilimo, utekelezaji wa miradi ya ujenzi, maboresho katika usafirishaji na ugavi, nishati ya uhakika, pamoja na utekelezaji wa sera za fedha na kibajeti". Amesema 

Amesema mfumuko wa bei uliendelea kuwa tulivu katika kipindi chote cha mwaka 2024, ukiwa chini ya lengo la asilimia 5 kwa Tanzania Bara na kukaribia lengo hilo kwa upande wa Zanzibar. 

Tutuba amesema katika robo ya nne ya mwaka 2024, mfumuko wa bei kwa Tanzania Bara ulikuwa wastani wa asilimia 3 kutokana na upatikanaji wa chakula cha kutosha, utekelezaji wa sera thabiti za fedha na bajeti, na kupungua kwa bei za bidhaa katika soko la dunia, hususan mafuta ghafi. 

Vilevile amesema kwa upande wa Zanzibar, mfumuko wa bei ulipungua hadi asilimia 4.5 mwezi Novemba 2024.

"Mfumuko wa bei unatarajiwa kuendelea kuwa tulivu katika robo ya kwanza ya mwaka 2025, ukibakia katika viwango vya kati ya asilimia 3.1 na asilimia 4.  Hali hii itatokana na kuendelea kuwepo kwa chakula cha kutosha, utulivu wa thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni, umeme wa uhakika, na kushuka kwa bei za bidhaa katika soko la dunia, hususan mafuta ghafi. 

Pamoja na hayo Gavana Tutuba amesema thamani ya shilingi inatarajiwa kuwa imara katika robo ya kwanza ya mwaka 2025, kutokana na kuwepo kwa ukwasi wa kutosha wa fedha za kigeni uliopatikana katika robo ya nne ya mwaka 2024, utekelezaji wa sera ya fedha kutokana, uamuzi wa kubakiza Riba ya Benki Kuu kuwa asilimia 6, na bei za bidhaa katika soko la dunia kuwa nafuu.

Amesema Benki Kuu inatarajia kuendelea kuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni, na kuongeza fedha za kigeni pale itapohitajika. Akiba iliyopo sasa ni zaidi ya dola za Marekani bilioni 5.5, kiwango ambacho kinatosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa zaidi ya miezi 4.7.

"Akiba hiyo inatarajiwa kubaki katika kiwango hicho katika robo ya kwanza ya mwaka 2025 kutokana na juhudi zinazofanywa na Benki kuu katika kuongeza akiba ya fedha za kigeni, ikiwemo kununua dhahabu hapa nchini". Ameeleza Gavana Tutuba.

Sanjari na hayo amesema deni la Taifa liliendelea kuwa himilivu, ambapo kwa mwaka 2023/24 lilikuwa takriban asilimia 41.1 ya Pato la Taifa (GDP) kwa thamani halisi ya sasa (NPV). 

Kiwango hiki kilikua chini ya ukomo wa uhimilivu wa nchi na kigezo cha mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) cha asilimia 55 na asilimia 50, mtawalia".  Amesema

Amesema kwa kuzingatia thamani ya bei za sasa, deni la Taifa lilikuwa asilimia 46.1 ya Pato la Taifa, chini ya kigezo cha mtangamano kwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) cha ukomo wa asilimia 60.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba akiwasilisha mrejesho wa kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu ya Tanzania kwa Wakuu wa Taasisi za kifedha nchini ambayo ilifanya kikao chake cha kila robo mwaka Januari 7, 2025 na kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini. Tukio hilo limefanyika leo Januari 8, 2024 katika Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba akiwasilisha mrejesho wa kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu ya Tanzania kwa Wakuu wa Taasisi za kifedha nchini ambayo ilifanya kikao chake cha kila robo mwaka Januari 7, 2025 na kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini. Tukio hilo limefanyika leo Januari 8, 2024 katika Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba akiwasilisha mrejesho wa kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu ya Tanzania kwa Wakuu wa Taasisi za kifedha nchini ambayo ilifanya kikao chake cha kila robo mwaka Januari 7, 2025 na kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini. Tukio hilo limefanyika leo Januari 8, 2024 katika Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba akiwasilisha mrejesho wa kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu ya Tanzania kwa Wakuu wa Taasisi za kifedha nchini ambayo ilifanya kikao chake cha kila robo mwaka Januari 7, 2025 na kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini. Tukio hilo limefanyika leo Januari 8, 2024 katika Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa Taasisi za Kifedha nchini wakipata mrejesho wa kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu ya Tanzania ambayo ilifanya kikao chake cha kila robo mwaka Januari 7, 2025 na kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini. Tukio hilo limefanyika leo Januari 8, 2024 katika Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa Taasisi za Kifedha nchini wakipata mrejesho wa kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu ya Tanzania ambayo ilifanya kikao chake cha kila robo mwaka Januari 7, 2025 na kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini. Tukio hilo limefanyika leo Januari 8, 2024 katika Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa Taasisi za Kifedha nchini wakipata mrejesho wa kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu ya Tanzania ambayo ilifanya kikao chake cha kila robo mwaka Januari 7, 2025 na kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini. Tukio hilo limefanyika leo Januari 8, 2024 katika Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa Taasisi za Kifedha nchini wakipata mrejesho wa kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu ya Tanzania ambayo ilifanya kikao chake cha kila robo mwaka Januari 7, 2025 na kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini. Tukio hilo limefanyika leo Januari 8, 2024 katika Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa Taasisi za Kifedha nchini wakipata mrejesho wa kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu ya Tanzania ambayo ilifanya kikao chake cha kila robo mwaka Januari 7, 2025 na kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini. Tukio hilo limefanyika leo Januari 8, 2024 katika Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

at 4:52 PM 0 comments
Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook
Older Posts Home

Popular Posts

  • UKAHABA WA KUTISHA WAIBUKA KIGAMBONI DAR ES SALAAM
  • TV1 KURUSHA LIVE LIGI KUU YA UINGEREZA 'PREMIERE LEAGUE' BURE
  • UCHUNGUZI KUTOKA POLISI: Jacky Daniel" imechangia kifo cha Kanumba
  • LIVEEE MUDA HUU MSANII WEMA SEPETU AZIMIA NA ANAKIMBIZWA HOSPITAL KWA SASA
  • JUST IN:TAARIFA TULIZO ZIPATA MPAKA SASA KUHUSU KIFO CHA MWIGIZAJI STEVEN KANUMBA...
Powered by Blogger.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Blog Archive

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa